Watu 60 watengwa kutokana na homa ya tumbili Nigeria

ZAKACHEKA.BLOGSPOT.COM
30 OKTOBA 2017
Watu 60 watengwa kutokana na homa ya tumbili NigeriaWatu 60 wametengwa katika jimbo lililo kaskazini mwa Nigeria la Kano, baada ya kukaribiana na watu wanakosiwa kuugua homa ya tumbili au monkeypox.

Kamishia wa afya katika jimbo la Kano, Kabul Gesto, alisema kwau moja ya dalili za ugonjwa huo iligunduliwa kwenye mgongwa lakini akasema kuwa ugonjwa huo huenda ukawa homa ya ndege.
"Hadi pale matokeo ya sampuni za damu yaliyotumwa kwenda mji mkuu Abuja yatakaporudishwa, hiki kitakuwa kisa cha kushukiwa," alisema 
Dr Getso anasema kuwa wagonjwa 11 katika majimbo 36 nchini Nigeria wameathirika na homa ya tumbuli.
Mamlaka za afya nchini Nigeria zimekuwa zikionya dhdi ya ulaji wa tumbili na nyama ya msituni wiki chache zilizopita.
Waziri wa afya Isaac Adewole anasema katika taarifa ya hivi punde kuwa licha ya tiba ya ugonjw ahuo kutujulikana hakuma wasi wasi kwa sababu homa hiyo siyo hatari.
Hata hivyo amewashauri watu kuchukua tahadhari ikiwemo kujiepusha na maeneo yenye misongamano.
Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: