Trump: Japan itayatungua makombora ya Korea Kaskazini

ZAKACHEKA.BLOGSPOT.COM
6 Nov 2017
Bwa. Trump na mwenyeji wake Shinzo Abe, katika ziara yake ya kwanza nchini Japan na Bara Asia kama Rais wa Marekani
Bwa. Trump na mwenyeji wake Shinzo Abe, katika ziara yake ya kwanza nchini Japan na Bara Asia kama Rais wa Marekani

Rais wa Marekani Donald Trump, amesema kwamba Japan itatungua makombora ya Korea Kaskazini, kwa kutumia mitambo ya kijeshi iliyonunuliwa kutoka Marekani.
Wakati huo huo, waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe, amesema kwamba, taifa lake litatungua makombora hayo kabla ya kutua ardhini, "ikiwa hilo litahitajika".
Viongozi hao wawili, walisema hayo walipozungumza na waandishi habari wakati wa kumalizika rasmi kwa ziara ya kwanza ya kitaifa ya Bwana Trump nchini Japan.
Katika miezi ya hivi karibuni, Korea Kaskazini imerusha makombora mawili hatari juu ya mipaka ya Japan.
Trump aapa kukabiliana na Korea Kaskazini kwenye ziara yake ya Bara Asia.
Alipokuwa akijibu maswali ya waandishi habari leo Jumatatu, Bw Trump alisema kwamba, Bwana Abe atanunua "kiasi kikubwa cha zana za kivita" kutoka Marekani.
Akigusia zana hatari za kinuklea za Korea Kaskazini, Trump alisema kuwa Bw Abe "atazishambulia zikiwa bado angani" mara tu atakapokuwa amemaliza kununua silaha hizo za kijeshi, anazosema kuwa itatoa ajira ya kazi kwa Wamarekani na pia "kutoa usalama kwa Japan".
Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: