Aanguka kutoka ghorofa ya 62 na kufariki

ZAKACHEKA.BLOGSPOT.COM=>
Mwezi uliopita, Wu Yongning alielekea kufanya anachopenda kufanya - kuparaga orofa za majengo makubwa bila ya vifaa vyovyote vya usalama na hujipiga video akining'inia kutoka juu ya mjengo hayo kwa vidole vyake tu vya mkononi.
Kilichofuata baada ya hapo pengine sio jambo la kushtusha - raia huyo wa Kichina alianguka orofa 62 kutoka juu na kufariki papo hapo.
Maelfu ya wafuasi wake walishikwa na wasiwasi alipoacha kuweka video za vituko vyake katika mitandao kama vile Huoshan na Kuaishou, lakini kifo chake kilithibitishwa katika siku chache tu za hivi karibuni, kwanza na mpenzi wake baadaye likafuata tangazo la kmaafisa wa utawala.
Kanda ya video ya kushtusha ya kilichoonekana kuwa muda wake wa mwisho wa uhai - jaribio lake la kuparaga kuta za orofa hiyo katika mji wa Changsha city - ilianza kusambaa katika mtandao wiki hii.
Kifo chake kimezusha maswali mengi ya wasiwasi na ya kutafakari kuhusu kuhatarisha maisha katika kutafuta pesa "cash for clips" sekta ya kusambaza video za aina hiyo katika mitandao.
Maswali sasa yanaulizwa, kuhusu iwapo majukwaa haya katika mitandao na watazamaji wake ndiyo yanayohusika kwa kifo chake.
• Tuma habari picha na video za matukio mbalimbali WhatsApp kwa 0625966236
Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: