KAIMU Balozi wa Marekani nchini, Dk Inmi Patterson (pichani) amesema Serikali ya Marekani inaona fahari kufanya kazi na Watanzania huku ikiunga mkono jitihada za wananchi kujenga Tanzania yenye amani, ustawi, usalama na afya.
Alisema hayo katika ziara yake mkoani Mwanza Novemba 26 hadi 28, mwaka huu, iliyolenga kukuza uelewa wa wananchi kuhusu jitihada zinazofanywa na Marekani kujenga uwezo wa Watanzania katika kujenga jamii zenye afya, kukuza uchumi wa jamii na mkoa na kusaidia katika elimu.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania, Kaimu Balozi aliyasema hayo akiwa katika Shule ya Wauguzi ya Askofu Anthony Mayalla iliyopo katika Hospitali ya Bugando jijini Mwanza.
Katika shule hiyo, wauguzi wa Kimarekani wanafanya kazi na kuwafundisha wenzao wa Kitanzania mbinu za kuwahudumia watoto wachanga na akina mama waliojifungua kama sehemu ya mpango wa ubia wa kutoa huduma za afya duniani.
“Uhusiano wetu mkubwa unaakisiwa na ushirikiano wa kina baina ya nchi zetu na nina imani kuwa, tutaendelea kuimarisha uhusiano huu wa kihistoria tunapoendelea kusaidiana,” alisema.
•Tuma habari picha na video za matukio mbalimbali WhatsApp kwa 0625966236
0 Post a Comment:
Post a Comment