California: Maporomoko ya ardhi yaua watu 13 Marekani

ZAKACHEKA.BLOGSPOT.COM=>

Watu 13 wamefariki kutokana na maporomoko ya ardhi yaliyosababishwa na mvua kubwa kusini mwa jimbo la California, Marekani, maafisa wamesema.
Wengine 163 wamelazwa hospitali, 20 wakiwa na majeraha yanayohusiana na mvua kubwa.
Wanne wana majeraha mabaya.
Watu wapatao 300 wanadaiwa kukwamba katika hori ya Romero, mashariki mwa mji wa Santa Barbara.
Polisi wamesema eneo lililokumbwa na maporomoko hayo linafanana na "uwanja wa vita wakati wa Vita Vikuu vya Kwanza vya Dunia".
Mafuriko na maporomoko ya ardhi yameathiri baadhi ya maeneo ambayo yaliathiriwa na moto mkubwa wa nyika na yameharibu barabara kuu ya pwani umbali wa maili 30 (48km).
Maafisa wa uokoaji wamesema kuna watu kadha ambao hawajulikani waliko na kwamba idadi ya waliofariki inatarajiwa kupanda.
Maafisa wa Kikosi cha Ulinzi Baharini wametuma ndege kadha kusaidia juhudi za uokoaji na wametahadharisha umma dhidi ya kutumia ndege zisizo na marubani kwani zitatatiza juhudi za uokoaji.
Maelfu ya wakazi wa California waliamrishwa kuondoka makwao Jumatatu, mara ya pili katika kipindi cha miezi miwili. Mara ya kwanza ilikuwa ni kwa sababu ya moto, wakati huu ni kwa sababu ya mvua.
*Wasiliana nami kwa 0625966236*
Tembelea blog hii kwa www.Zakacheka.blogspot.com
Pia tembelea blog ya neno la Mungu kwa www.Zakachekainjili.blogspot.com
Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: