Korea Kaskazini na Kusini kufanya mazungumzo ya kijeshi ili kuondoa wasiwasi

ZAKACHEKA.BLOGSPOT.COM=>
Korea Kaskazini na Kusini zimekubaliana kufanya mazungumzo ya kijeshi ili kuondoa wasiwasi uliopo mipakani baada ya mkutano wa kwanza katika kipindi cha miaka miwili.
Korea Kaskazini pia itatuma ujumbe katika michezo hiyo ya msimu wa baridi itakayofanyika Korea Kusini mnamo mwezi Februari.
Makubaliano yaliafikiwa kurudisha nambari ya simu ya jeshi ilioondolewa mwaka mmoja uliopita , kulingana na serikali ya Korea Kusini.
Hatahivyo ujumbe wa Korea Kaskazini ulipinga ajenda ya kusitisha mpango wa kinyuklia , Korea Kusini iliongezea.
Marekani iliunga mkono kufanyika kwa mkutano huo.
Idara ya maswala ya kigeni ilisema kuwa Marekani inaendelea na majadiliano na maafisa wa Korea Kusini ambao watahakikisha kuwa kishiriki kwa Korea Kaskazini katika michezo ya Olimpiki hakutakiuka kivyovyote vikwazo vya Umoja wa mataifa.
Baada ya siku moja ya mazungumzo , pande zote mbili zilitoa taarifa ya pamoja ambayo ilithibitisha kuwa wamekubaliana kufanya mazungumzo ya kijeshi ya kuondoa wasiwasi uliopo.
Korea Kaskazini pia ilikubali kutuma kikosi cha michezo ya Olimpiki ikiwemo, wanariadha, mashabiki, wawakilishi wa sanaa, na kikosi cha kuonyesha mchezo wa Takweondo mbali na vyombo vya habari katika michezo hiyo huku Korea Kusini ikikubali kutoa vifaa na huduma zote za kikosi hicho.
Taarifa hiyo pia ilizungumzo kuhusu mabadilishano ya mawazo mbali na mazungumzo ya ngazi za juu kuhusu kuimarisha uhusiano wa mataifa hayo mawili kulingana na chombo cha habari cha Korea Kusini cha Yonhap.
*Wasiliana nami Zachary John Bequeker kwa 0625966236*
Tembelea blog hii kwa www.Zakacheka.blogspot.com
Pia tembelea blog ya neno la Mungu kwa www.Zakachekainjili.blogspot.com
Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: