Mfungwa aliyedaiwa kufariki azinduka akiwa chumba cha kuhifadhia maiti Uhispania

ZAKACHEKA.BLOGSPOT.COM=>

Mfungwa mmoja kaskazini mwa Uhispania alizinduka na kujipata akiwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti baada ya kuthibitishwa kwamba alikuwa amefariki na madaktari watatu, vyombo vya habari Uhispania vinasema.
Gonzalo Montoya Jiménez alikuwa anazuiliwa katika gereza moja jimbo la Asturias na alizinduka saa chache tu kabla yake kufanyiwa upasuaji wa kubainisha chanzo cha kifo chake.
Mwili wake tayari ulikuwa umechorwa alama tayari kwa upasuaji.
Kwa sasa, amewekwa chini ya uangalizi wa madaktari katika chumba cha wagonjwa mahututi hospitali ya Oviedo.
Mmoja wa jamaa zake ameambia gazeti la La Voz de Asturias kwamba Montoya "alikuwa na alama ya kufanyiwa upasuaji, tayari kupasuliwa".
Inadhaniwa kwamba hicho kilikuwa kisa cha hali iitwayo 'catalepsy' duru katika hospitali hiyo zimeambia runinga ya Telecinco ya Uhispania.
Catalepsy ni hali ambapo ishara muhimu za uhai kwenye mwili wa binadamu hufifia kiasi cha kutoweza kutambulika.
Hata hivyo, hili bado halijathibitishwa.

Kifo" chake kilikuwa kimethibitishwa na madaktari watatu gerezani ambao waliagiza mwili wake upelekwe kwenye ufuo kwa uchunguzi zaidi.
Mwili huo ulipelekwa ufuo wa Taasisi ya Matibabu ya Kisheria katika makao makuu ya jimbo Oviedo.
Wasiliana nami kwa 0625966236*
Tembelea blog hii kwa www.Zakacheka.blogspot.com
Pia tembelea blog ya neno la Mungu kwa www.zakachekainjili.blogspot.com
Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: