Kama umejichubua ama una michirizi ya mwili waweza kukosa ajira Ghana

ZAKACHEKA.BLOGSPOT.COM=>
Kitengo cha uhamiaji nchini Ghana kimewaondolea vigezo waliotuma maombi ya kazi wakati wa zoezi la kukusanya wafanyikazi wapya kwa sababu ya kubadilisha rangi ya miili yao ama maarufu kujichubua na wenye michirizi mwilini.
Msemaji wa kitengo hicho amesema kuwa wamewaondolea vigezo kwa sababu wanaweza kupata majeraha na kutokwa na damu wakati wa mafunzo.
Baadhi ya Waghana wamepinga hatua hiyo na kuiita ya kibaguzi huku baadhi wakikasirishwa zaidi na waliondolewa vigezo kwa sababu ya kuwa na michirizi mwilini.
Nao baadhi wamesifia hatua ya kuwaondelea vigezo waliobadili rangi zao za mwili.
Walioondolewa vigezo, wengine ni wenye michoro mwilini (tattoo) na wenye rasta.
Wanaotuma maombi ya kutraka ajira wanapitia vipimo vya mwili na afya kama sehemu ya zoezi la kuwachuja wenye vigezo.
Watu 84,000 walituma maombi ya kazi hiyo, huku wanaohitajika wakiwa ni 500 pekee.
*Wasiliana nami kwa 0625966236*
Pia tembelea blog ya neno la Mungu kwa: www.zakachekainjili.blogspot.com
Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: