SOMO: THAMANI YA MTAKATIFU

MHUBIRI: ASKOFU YUDAS KARUMBETE
MAHALI: FGBF MWANZA 14.01.2018
MWANDISHI: Zachary John Bequeker +255625966236
=================================


Tunapaswa kujihadhari na mafundisho yanayoeleza kwamba mtu anapokufa vikao hufanyika na kumpitisha mtu Fulani ni mtakatifu.

Utakatifu ni hapa hapa  duniani kabla mtu hajafa na Mungu anapendezwa na watakatifu waliopo hapa hapa duniani (ZABURI 16:3).

Kila anayeitwa "Mkristo" ni lazima awe mtakatifu ili aweze kwenda mbinguni (WAEBRANIA 12:14). Mungu ni mtakatifu nasi tunapaswa kuwa watakatifu(1 PETRO 1:15-16).

Paulo mtume alifunuliwa na Mungu kuwa utakatifu ni hapa duniani, na kwa sababu hiyo katika kuandika Nyaraka zake kwa Wakristo wa eneo Fulani aliwaita Watakatifu (TITO 2:11-12), (WAEFESO 1:1),(WAFILIPI 1:1),(WAKOLOSAI 1:1-2) Wote hao Paulo anaowaita watakatifu walikuwa hapa hapa duniani.

Watu wengi hawawezi kujiita watakatifu kwa sababu wanachanganya mambo.

 Nyakati za kanisa la kwanza kila mmoja alijua alipaswa kuwa mtakatifu na kimsingi makanisa yalikuwa ni ya watakatifu. Baada ya kuzaliwa kwa mwili inatakiwa kuzaliwa kwa Roho.

Kabla ya kuwa mtakatifu ni lazima kutubu dhambi na kumaanisha kuziacha; ni vyema kutubu hadharani kama ZAKAYO. Mwanzo wa wokovu lazima uwe na nina ya kumwona YESU kama ZAKAYO alipoamua kumwona Yesu.

Tunapokutana na Yesu tunapata wokovu (LUKA 19:1-10).

Baada ya mtu kuwa ameokoka anapewa uwezo wa kushinda dhambi za kutenda za nje na Si za ndani, na kwa mantiki hiyo unaweza kumuona mtu ameokoka, hafanyi uzinzi kwa nje lakini anafanya uzinzi moyoni, anapokaona kabinti kanakatiza mbele zake anakamezea mate; tatizo hapa ni UTAKASO.

 Utakaso unapokuja kwa mtu anapewa uwezo wa kushinda dhambi katika mwenendo wote. Utakatifu ni kuwa kama Kristo katika nia, mawazo, moyo na matendo.Mungu anaangalia ndani vile unavyotenda ndivyo iwe kuwaza Kwako.

 Utakaso unamfanya mtu awe na Moyo safi, na wenye moyo safi ndio watakaomwona Mungu (MATHAYO 5:8). Unapokuwa umetakaswa, tayari unakuwa mtakatifu, huna haja kusubiri tangazo Fulani au kikao Fulani kupitishwa kuwa mtakatifu.

Mtu asipojua thamani ya utakatifu shetani humchezea sana (HOSEA 4:6), Tunapoifahamu kweli tunawekwa huru (YOHANA 8:32).

Ni muhimu kujua uthamani wa mtakatifu, unapojua utauishi sawasawa; kitu usichokijua unaweza ukakosa haki yako ya msingi. Mfano mtu anapokuwa amekata tikiti"ticket " ya ndege, anakuwa na haki ya kula na kunywa kwa ndege ile wakati wa safari bila gharama zozote zile, mtu ambaye hafahamu hivyo, hostess anapopita na kumuulize kipi amletee utasikia anasema "it's OK with me" kumbe kaogopa akidhani atadaiwa gharama. Mtu anayejua ataagiza tena kwa maana anajua kuwa vinywaji vile na Chakula kile ni haki yake.

Hapo mwanzo tumesoma katika ZABURI 16:3 neno "bora" kwa biblia ya kiingereza ya KJV neno hilo linasomeka " Excellent " yaani "bora sana". Mtu aliye mtakatifu anaweza kuishi ndani ya sehemu yoyote ambayo watu wengi au karibu wote wanafanya dhambi yeye asifanye kwa sababu anajua alivyo wa thamani kwa Mungu.

Mtakatifu ni mtu wa heshima hivyo hapaswi kujilinganisha na watu wengine. Mtakatifu Si chombo cha udongo wala mti bali ni chombo cha thamani chenye heshima na kinachomfaa Bwana kwa kukitumia kwa kazi njema. Kila kitu cha thamani, chenye heshima hufanyiwa uangalizi wa hali ya juu.

Pamoja na kwamba watu na vitu vyote ni Mali ya Mungu, Mtakatifu ni "Tunu' (KUTOKA 19:5-6) katika biblia ya kiingereza ya KJV neno hilo linasomeka " peculiar treasure " yaani hazina ya pekee iliyo yatofauti kwa Mungu wetu. Mtu mtakatifu hawezi kufikiwa na mapepo kwa sababu ana maximum security, yaani ulinzi wa hali ya juu zaidi ya Rais yeyote duniani, malaika ndiyo walinzi na kwa hesabu ya malaika mmoja anaweza kuteketezamaadui 185,000. Kifo cha mtakatifu kinapangwa na Bwana mwenyewe na Si mwanadamu.

Mtakatifu anapoomba maombi yake husikiwa na Mungu kwa haraka sana.

 Mtakatifu amdchaguliwa kuwa mtu wa Mungu (KUMBUKUMBU LA TORATI 14:1-2) katika biblia ya KJV neno " peculiar people" limetumika. Tunapoishi maisha ya utakatifu kwa kujitoa kutumika Mungu hawezi kutuacha tuaibike kwani tunapoaibika sisi anakuwa na yeye(Mungu) ameaibika, na kawaida Mungu hawezi kukubali kuaibika.Mungu hujionea fahari juu ya watakatifu wake.

 Shetani anajua mtu akiwa mtakatifu anakuwa amezingirwa akilindwa na kubarikiwa na Mungu na hatoweza kumdhuru kwa sababu hiyo Shetani huwazuia watu kuishi maisha ya utakatifu ili aendelee kuwatesa, Hebu shituka Leo katika Jina la Yesu, sema Amen. Baada ya kuokoka Mungu huweka roho ya ujasiri ndani yetu. Hivyo kazi anayoifanya shetani ni kuweka roho ya woga ndani yetu ya kuona kuwa watakatifu hapa duniani ni kazi ngumu na haiwezekani ili aendelww kututesa. Tumwombe Mungu atutakase kwani ni ahadi yake kwetu.
Kama hujaokoka , lazima kuokoka kisha uombe UTAKASO.

Written by Ev. Zachary John Bequeker from MWANZA +255625966236
Tembelea www.zakachekainjili.blogspot.com
Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: