Avani Chaturvedi, 24, amekuwa mwanamke kwa kwanza kuendesha ndege ya vita akiwa peke yake nchini India.
Aliendesha ndege ya Mig-21 Bison kwa dakika 30 mapema wiki hii, kwa mujibu wa jeshi la wanahewa la India.
"Aliitaja siku hiyo kuwa ya kihistoria katika jeshi la India, msemaji Anupam Banerjee alisema.
Bi Chaturvedi alikuwa miongoni mwa wanawake watatu wa kwanza marubani wa ndege za vita kujumuishwa katika jeshi la wanahewa la India.
Jeshi la wanahewa lilichapisha picha yake akisimama karibu ndege ya vita.
Bi Chaturvedi alifuzu mwezi Juni mwaka 2016 pamoja na wanawake wengine wawili Bhawana Kanth na Mohana Singh, ambao watandesha ndege kama hiyo hivi karibuni kama shemu ya mafuzo.
Kabala ya mwaka 2016 wanawake walichuakua asilimia 2.5 ya jeshi la India walifanya kazi tu katika maeneo yasiyohusu vita.
Taifa jirani la Pakistan lina karibu wanawake 20 marubania wa ndege za vita. Jeshi la Pakistam lilianza kuwafunza wanawake majukumu ya vita mwaka 2006.
0 Post a Comment:
Post a Comment