Kenya: Wabunge wajadili 'ukosefu wa karatasi za kwenda haja kubwa' bungeni

ZAKACHEKA.BLOGSPOT.COM=>
Wakenya wamewataka wabunge wao kubeba karatasi zao za kutumia baada ya haja kubwa bungeni iwapo wameghadhabishwa na ukosefu wa karatasi hizo bungeni.
Wabunge katika mjadala siku ya Jumatano walitumia muda wao mwingi kulalamikia ukosefu wa karatasi hizo na maji katika vyoo vyao.
Ni swala lililowaunganisha wabunge wa chama tawala na wale wa upinzani.
Kiongozi wa walio wachache bungeni John Mbadi alisema kwamba sio maji pekee ambayo hakuna bali hata karatasi hizo.
''Huwezi kuniambia kwamba bunge ambalo wabunge wa taifa wanafanya kazi zao halina karatasi za kwendea haja kubwa na kwamba mara nyengine unaingia chooni na hakuna karatasi hizo''.
Mbadi aliongezea kwamba swala hilo la choo ni tete mno huku mifereji pia ikikosa maji hivyobasi kuwa vigumu kwa wabunge kutekeleza wajibu muhimu wa kuwa wasafi.
''Mwanzo katika jumba la Continental House unafaa kuwa makini sana , unafaa kuangalia iwapo kuna maji kwa sababu unaweza kujichafua....kabla ya kuchukua hatua yoyote ni lazima uhakikishe kwamba kuna maji katika mifereji. Kwa sababu unahitaji maji hayo baada ya kufanya mambo fulani'', aliongezea Mbaddi.
Kiranja wa walio wachache bungeni ambaye pia ni mbunge wa Suna Mashariki Junet Mohammed aliishutumu kamati ya maandalizi katika bunge la 11 kwa kushindwa kuimarisha hali ya wabunge licha ya kusafiri katika mataifa kadhaa ikiwemo Uganda ili kujifahamisha.
''Bwana Spika chai inayotolewa hapa haina maziwa na inafanana na ile inayotolewa wakati wa matanga'', alisema katika matamshi yaliozua kicheko kutoka kwa wabunge wenzake.
Mbunge wa Nambale Sakwa Bunyasi alisema kuwa bunge halihitaji wapishi pekee bali wapishi wataalam ambao wanaweza kupika vyakula vizuri.
Naye naibu kiongozi wa walio wengi bungeni Jimmy Angwenyi alisema kuwa kuna umuhimu wa idara ya upishi kuimarisha upikaji wa vyakula.
''Naamini kwamba tuliwaajiri watu wanaofaa kupika chakula kizuri.Sifai kupiga foleini kwa muda mrefu kwa sababu mimi ni mzee naweza kuzirai'' , alisema Angwenyi.
''Bwana Spika sio haki kwamba baadhi ya maeneo ya kuegesha magari yaliotengewa wabunge yamechukuliwa na maafisa wengine.hatuwezi kuingia katika eneo la kufanyia mazoezi tunapohitaji''.
Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: