Kiongozi wa Mtandao wa wanafunzi Tanzania Abdul Nondo atoweka

Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP) umesema mwenyekiti wake Mahmud Abdul Ormari Nondo hajulikani alipo na kulitaka jeshi la polisi kuhakikisha anapatikana akiwa salama kwa haraka.
Baba mdogo wa kiongozi huyo Mussa Mitumba akiwahutubia wanahabari pia ametoa wito kwa 'mwanawe' kurudishwa akiwa hai aendelee na kutafuta kutimiza ndoto zake.
Kiongozi huyo wa wanafunzi alionekana mara ya mwisho mnamo Jumanne katika afisi za shirika hilo eneo la Sinza, Dar es Salaam alipokuwa akitoa ufafanuzi kuhusu taarifa iliyokuwa imetolewa na shirikisho la vyuo vikuu nchini humo, Tahliso.
"Ghafla katika hali ya kutatanisha, kuanzia saa 6 hadi saa 8 usiku alijitoa kwenye makundi yote ya mtandao wa kijamii wa WhatsApp jambo lililozua taharuki miongoni mwa watu wengi na kuanza kutaka kujua nini kimemsibu," muungano huo umesema kupitia taarifa.
"Saa 9.09 usiku alituma ujumbe mfupi kwa Mkurugenzi wa Idara ya Sheria TSNP Paul Kisabo ujumbe uliosomeka 'Am at risk!' [Nimo hatarini]."
Muungano huo umesema juhudi za kuwasiliana naye kwa simu kufikia sasa bado hazijafanikiwa.
Wamesema wamepiga ripoti kwa jeshi la polisi katika kituo cha chuo kikuu cha Dar es Salaam.
Taarifa ya chama hicho cha wanafunzi inasema Bw Nondo amekuwa akipokea vitisho kutoka kwa watu wasiojulikana.
Wakati mmoja, anadaiwa kukamatwa na askari wa jeshi la polisi eneo la Milimani City na kutuhumiwa kwamba "analeta uchochezi wa baadhi ya wanafunzi waliokosa mikopo ya elimu ya juu kuandamana."
"Mara kadhaa kumekwua na makundi ya watu asiowatambua na wenye nguo za kiraia wakijitambulisha kama watu wa usalama ambao wamekuwa wakimfuatilia na kumpa vitisho hivyo," taarifa hiyo inasema.
Muungano huo umesema viongozi mbalimbali wa TSNP wamekuwa wakipokea vitisho tofauti tofauti.
Muungano wa Mashirika ya Kutetea haki za kibinadamu Tanzania (THRDC) pia wametoa wito kwa polisi kufanya uchunguzi na kuhakikisha Bw Nondo anapatikana akiwa salama.
"Kutoweka kwa Abdul huenda kunahusiana na kazi yake katika kutetea haki za kibinadamu," imesema taarifa iliyotolewa na mratibu wa kitaifa wa THRDC Onesmo Olengurumwa.

Download App YETU hapa⬇⬇

Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: