Mwanamke awakomboa wafanyabiashara ndogondogo

Mwanamke aliyejitambulisha kwa jina  moja la Avintishi, leo amejitoa kimasomaso na kumueleza Rais John Magufuli kuhusu kero wanayopata wafanyabiashara ndogondogo ikiwamo kunyang’anywa bidhaa zao.

 Mama huyo alimwambia Rais Magufuli leo, Machi 15 katika uzinduzi wa kiwanda cha Sigara cha Philip Morris, Morogoro.

“Wanatunyang’anya bidhaa zetu, na sisi hatuna mtu wa kutusaidia, wanapochukua, wanatutoza fedha na wanachukua bidhaa. Na umri huu hatuwawezi vijana wadogo,” alisema mama huyo.

Baada ya kueleza hayo, Rais alimuita Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro, John Mugarula kujibu kero zilizoibuliwa na mama huyo.
Mkurugenzi huyo, alisema wanawaondoa wafanyabiashara hao kwa sababu wametengewa maeneo maalumu na aliibua pia  suala la kipindupindu kuwa ni sababu ya kuwaondoa wafanyabiashara hao.

 Baada ya hapo Rais, alimuhoji mama huyo, ni kiasi gani alitozwa na askari mgambo wa manispaa, mama huyo akaeleza kuwa alitozwa Sh200, 000.

Rais alihoji tena, iwapo mama huyo anamkumbuka askari mgambo aliyemtoza kiasi hicho?

“Kwa sababu ya kitete na woga, siwezi kumkumbuka,” amejibu mama huyo.

Baada ya kusema hayo, Rais alimpa mama huyo fedha na kumtaka mkurugenzi kumpa kiasi kingine cha fedha mama huyo.

Kadhalika, Rais aliagiza kuanzia leo, wafanyabiashara hao wasibughudhiwe kwa sababu ni watoto wa maskini.

 Wageni wengine waliokuwapo katika uzinduzi huo, akiwamo Mbunge wa Viti Maalumu, (CCM) Getrude Rwakatare, waliinuka na kumchangia fedha mama huyo.

Download App YETU hapa⬇⬇



Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: