Bodi ya madaktari nchini Kenya imeitaja zahanati ambayo mwanamke mmoja alifanyiwa upasuaji wa kuongeza maziwa yake kabla ya kufariki , kwa mujibu wa gazeti la nchini Kenya la Daily Nation.
Afisa mkuu wa bodi hiyo Daniel Yumbya amesema ni zahanati ya Surgeoderm Healthcare iliyo Nairobi, iliohusika na kisa hicho kilichosababisha cha Bi June Wanza wiki iliyopita.
Bw Yumbya alisema bodi hiyo ilikuwa imeiandikia zahanati hiyo kutaka ieleze sababu zilizosababisha mwanamke huyo alazwe kwenye hospitali ya Nairobi ambapo alifariki.
Pia imeomba ripoti kutoka kwa Hospitali ya Nairobi.
Zahanati hiyo iliyo barabara ya Thata mtaa wa Kilimani mjini Nairobi imeweka matangazo kwenye mtandao wake kuelezea huduma inazotoa ukiwemo upasuaji huo wa kuongeza au kupunguza maziwa.
Bi Wanza alifanyiwa upasuaji wa kuongeza maziwa yake lakini akakumbwa na matatizo ya kiafya.
Kisha alienda kutafuta usaidizi wa matibabu kwenye hospitali ya Nairobi siku ya Jumatano kabla ya kufariki siku ya Alhamisi wiki iliyopita.
Gazeti la Daily Nation lilisema kuwa madaktari walijaribu kumuokoa Bi Wanza baada ya kugundua kuwa sehemu ya utumbo wake ilikuwa imekatwa kufuatia upasuaji huo.
Na Mwandishi Wetu: Zachary John Bequeker
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 Post a Comment:
Post a Comment