Ukatili: Mtoto achomwa makalio


Mtoto mwenye umri wa miaka {11}amechomwa moto makalioni na kufungiwa ndani kwa muda wa siku mbili kwa kosa la kuiba pesa kiasi cha shilingi elf tano kitendo ambacho ni cha kikatili katika maisha yake .

Mtoto huyo   anayesoma darasa la tatu  katika shule ya msingi Mwinyi iliyopo mkoani Tabora jina limehifadhiwa  amefanyiwa ukatili huo siku ya jumatatu ya tarehe 11  /06 /2018 akiwa kwa baba yake mdogo wilayani kahama.

 Akizungumza na kituo hiki Mtendaji wa mtaa wa nyihogo Bwn.Antony Costa  amesema kuwa amepata taarifa kutoka kwa mwenyekiti pamoja na majirani wa familia hiyo na kuwa mtuhumiwa wa kosa hilo bado hajakamatwa

'Nilipata taarifa za tukio hilo kutoka kwa mwenyekiti wa mtaa na majirani na ndiponilipofika eneo la tukio na mtuhumiwa hajakamatwa "alisema Costa. .….

Pia msemaji wa Dawati La Jinsia wilayani Kahama mkoani shinyanga Bi . Jenny Joakim Eras  amekili kupokea  tukio la mtoto huyo ofisi kwake na kuwa mtoto anaendelea na matibabu katika hospitali ya halmashauri ya mji wa kahama .

Eras  ametoa ushauri kwa wanajamii  kuwa na malezi bora kwa watoto woa kwa kuzingatia sheria ya mtoto ya mwaka 2009. .
Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: