Raia wa Marekani akamatwa Korea Kaskazini


Msukosuko ni mkubwa kufuatia maonyesho makubwa ya zana za kivitaShirika la habari la Korea Kusini linasema kwamba raia wa tatu wa Marekani ametiwa mbaroni nchini Korea Kaskazini.
Bila kutaja vyanzo vyake, shirika hilo linasema mwanamume huyo mwenye asili ya kimarekani na kikorea alikamatwa akiwa kwenye uwanja wa ndege akijaribu kuondoka Pyongyang.
Inaarifiwa kwamba mwanamume huyo ni mhadhiri wa zamani wa chuo kikuu cha Yanbian Uchina, na alikuwa korrea kaskazini kwa kipindi cha mwezi mmoja kwa shughuli za uhisani.
Serikali za korea kusini na kaskazini hazijadhibitisha madai hayo.
Raia wengine wawili wa Marekani wanazuiliwa nchini humo.
Korea kaskazini ilifanya maonyesho makubwa ya zana za kivita.


N korea parade april 2017
Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: