20 Mei 2017
Bado haijabainika iwapo Assange anaweza kuondoka ubalozi wa Ecuador jijini London bila kukamatwa
Mkuu wa mashtaka nchini Sweden ameamua kusitisha uchunguzi kuhusu madai ya ubakaji dhidi ya mwanzilishi wa mtandao wa Wikileaks Julian Assange.
Marianne Ny amesema kibali cha kukamatwa kwa Bw Assange kimebatilishwa kwa sasa kwani imekuwa vigumu kufikisha ilani ya kumkamata kwake.
bw Assange, 45, amekuwa akiishi katika ubalozi wa Ecuador jijini London tangu 2012, akihofia kukamatwa na kupelekwa Sweden kujibu mashtaka ambapo baadaye anaweza kupelekwa Marekani akajibu mashtaka zaidi.
Polisi jijini London wanasema bado watakuwa na wajibu wa kumkamata iwapo ataondoka katika ubalozi huo.
Polisi wa jiji la London wamesema Bw Assange bado anakabiliwa na shtaka ndogo la kukosa kujisalimisha wka mahakama, kosa ambalo anaweza kuadhibiwa kifungo cha hadi mwaka mmoja jela au kupigwa faini.
Uingereza haijasema lolote kuhusu iwapo imepokea ombi la kutaka kumpeleka Assange Marekani akajibu mashtaka.
Assange amekwua akitafutwa na Marekani kwa makosa ya kuvujisha maelfu ya nyaraka za siri kuhusu jeshi la Marekani na mabalozi wake.
Wakili wa Bw Assange jijini Sweden Per Samuelson amesema uamuzi wa mwendesha mashtaka Ijumaa ni "ushindi mkubwa" kwa mteja wake.
Marianne Ny amesema kesi hiyo inaweza kufufuliwa iwapo Assange atazuru Sweden kabla ya Agosti 2020
Mlalamishi katika kesi hiyo ya ubakaji hata hivyo ameshangazwa sana na uamuzi huo, wakili wake amesema, na kuongeza kwamba bado anadumisha madai yake dhidi ya Bw Assange, shirika la habari la AFP limesema.
0 Post a Comment:
Post a Comment