Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amesema hayo jana wakati akijibu swali la nyongeza la mbunge wa Viti Maalumu (Chadema), Lucy Owenya aliyetaka kujua kwa nini umeme umekuwa ukikatika mara kwa mara mkoani Kilimanjaro.
“Njia nyingi za umeme wetu ni zile zilizowekwa tangu mwaka 1964 , hivyo zimechoka, tunaendelea kutengeneza kidogo kidogo kwa kukata baadhi ya maeneo na kujenga kuliko kuzima umeme na kusubiri hadi tujenge,” amesema Profesa Muhongo.
Awali, katika swali la msingi mbunge huyo alitaka kujua sababu za umeme kukatika na lini tatizo hilo litakwisha.
0 Post a Comment:
Post a Comment