Wenye sifa kufurahia ajira


Rais Magufuli alisema hayo alipokuwa akipokea ripoti ya uhakiki wa vyeti feki mjini Dodoma baada ya kukamilika kwa uhakiki uliofanyika kwa miezi sita na watumishi 9,932 wakigundulika kutumia vyeti feki huku wengine 1,538 wakitumia cheti kimoja kwa zaidi ya mtu mmoja.
Akizungumzia suala hilo Mwenyekiti wa Umoja wa Maofisa Watendaji Wakuu wa Kampuni Binafsi nchini (CEOrt), Ali Mufuruki amesema kwa kufanya hivyo Serikali inaweka viwango bora vya elimu.
Pia, amesema inatoa nafasi kwa waliokuwa na elimu bora angalau kuingia kwenye soko la ajira, kwa sababu kuna nafasi zipo wazi zinazotakiwa kujazwa na wale tu wenye sifa.
 “Hii ni alarm hata kwa sisi sekta binafsi, kuliangalia hili kwa kina na kuongeza umakini wakati wa kuajiri, ”amesema Mufuruki.
Mufuruki anaungwa mkono na Profesa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(UDSM), Humphrey Moshi aliyesema waliofukuzwa watafungua mianya kwa wenye vyeti sahihi ambao hawajaajiriwa.
Mshirikishe Mwenzako: zakacheka.blogspot.com +255 625966236
Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: