8 Mei 2017
Kampuni ya kutengeneza madawa ya Johnson & Johnson (J&J), imeamrishwa na mahakama ya Marekani kulipa zaidi ya dola milioni 110 kwa mwamamke moja ambaye anasema kuwa alipata saratani ya uzazi, baada ya kutumia poda iliyotengenezwa na kampuni hiyo.
Lois Slemp mwenye umri wa miaka 62, kutoka Virginia alisema kuwa alipata saratani baada ya miongo minne ya kutumia poda ya talc.
Waendesha mashtaka wanasema kuwa kampuni hiyo haikutoa tahadhari kuhusu hatari ya mtu kupata saratani kutokana na bidhaa zake.
Wataalamu wanasema kuwa uhusiano kati ya poda hiyo na saratani haujathibitishwa huku J&J ikisema kuwa itakata rufaa.
Kesi hiyo ndiyo kubwa zaidi kuwai kuibuka katika ya kesi 2400 dhidi ya J&J kuhusu bidhaa zake za poda.
Bi Slemp kwa sasa anafanyiwa matibabu baada ya saratani hiyo iliyogunduliwa mwaka 2012 kusambaa hadi kwa ini lake.
0 Post a Comment:
Post a Comment