Shule ya Lucky Vicent yafungwa kwa siku saba, Samia Suluhu kuongoza kazi ya kuaga


 8 Mei 2017


 
Shule ya Lucky Vicent imefungwa kwa siku saba kufuatia vifo vya wanafunzi wake 32 vilivyotokea kwenye ajali ya gari jana Karatu.
Kutokana na ajali hiyo Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema na wabunge wengine wa Chadema wamefika shuleni hapo kutoa pole.
Lema kwa niaba wabunge wameeleza kusikitishwa na msiba huu na amewapa pole wafiwa lakini akatoa angalizo kusiingizwe siasa katika msiba huu mkubwa.
Meya wa jiji la Arusha Kalist Lazaro ameeleza kuwa Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, Waziri wa Tamisemi, George Simbachawene na Waziri wa Elimu, Profesa Joyce Ndalichako watafika jioni kuzungumza na wafiwa.
Leo Makamu wa Rais Samia Suluhu kwa niaba ya Rais John Magufuli ataongoza kazi  ya kuaga miili ya wanafunzi hao Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.
Mkuu wa shule hiyo, Ephraem Jackson hadi sasa vifo ni 36 na wanafunzi wawili bado wamelazwa Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru. Wanafunzi hao ni Sadiely Ismail na Wilson Tarimo.
Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: