Mabomu yasababisha zaidi ya watu 50,000 kuhama Ujerumani


8 Mei 2017

Mabomu kutoka vita vya pili vya dunia bado yako Hannover

Haki mil
Mabomu kutoka vita vya pili vya dunia bado yako Hannover.
0peresheni kubwa ya kuwaondoa wakaazi wengi wa mji wa Hanover ulioko kaskazini mwa Ujerumani, inaendelea, ya kuwahamisha zaidi ya watu elfu 50 baada ya mabomu makubwa ya wakati wa vita vya dunia, kupatikana kama hayajalipuka.
Wakaazi hao walitarajiwa kuondoka majumbani mwao jana, ili kuwapa nafasi wataalamu wa kutegua mabomu, kuhamishia mahala salama mabomu hayo ambayo yanakisiwa kuwa matano.
Operesheni hiyo itachukua siku nzima, na hata zaidi ikiwa mabomu mengineyatapatikana.
Washambuliaji walivamia mji wa Hanover mara 125 kwa mabomu, wakati wa vita vikuu vya pili vya dunia.
Wataalamu wanaamini kuwa mabomu ambayo hayakulipuka huenda yako chini ya jengo hili
Haki mili
Wataalamu wanaamini kuwa huenda mabomu ambayo hayakulipuka yako chini ya jengo hili.
Zaidi ya asilimia 20 ya mabomu yaliyoangushwa mjini humo hayakulipuka.
Baadhi ya mabomu mengine yalikuwa na vifaa vinavyochukua muda mrefu kulipuka, na ambayo kwa sasa yameanza kuoza, na kusababisha hatari kubwa.
Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: