Korea Kaskazini yalifanyia jaribio kombora la masafa marefu


14 Mei 2017

Korea Kaskazini ikionyesha zana zake
Haki miliki ya picha
Kumekuwa na shutma kubwa kote duniani dhidi ya hatua ya hivi punde ya Korea Kaskazini, kufanyia majaribio yake zana za nuklia
Marekani inataka vikwazo zaidi viongezewe taifa hilo huku Ikulu ya White House ikisema kuwa, Pyongyang imeachwa kutekeleza upumbavu kwa muda mrefu.
Rais mpya wa Korea Kusini Moon Jae-in, amelaani kitendo hicho cha Korea Kaskazini, cha kufanya majaribio zaidi ya zana zake za masafa marefu, akilitaja kama kitendo cha uchochezi.
Jeshi la Marekani limetihibtisha kuwa kombora hilo la masafa marefu, lilirushwa karibu na mji wa kaskazini magharibi wa Kusong na kuanguka katika bahari ya Japan.
Kombora hilo lilianguka katika bahari ya Japan
Moon ambaye alisema anataka ushirikiano zaidi na utawala wa Pyongyang, wakati wa kampeni yake, amejibu hatua hiyo kwa kuitisha mkutano wa dharura na washauri wake wa kiusalama.
Jaribio lingine la Korea Kaskazini la kuifanyia majaribio zana hizo, liligonga mwamba wiki mbili zilizopita.
Korea Kaskazini imekiuka maazimio ya Umoja wa Mataifa pamoja na vikwazo na kufanya majaribio matano ya zana zake za masafa marefu za nuklia.
Haki miliki ya pi
Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: