Mvua zaharibu Mazingira Tanga


13 Mei 2017


Moja ya barabara za Lushoto ambazo zimekumbwa
Moja ya barabara za Lushoto ambazo zimekumbwa na maporomoko na kusababisha uharibifu wa magari na miundombinu kwa ujumla 
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Thobias Mwilapwa alisema taarifa za athari zilizotokana na mafuriko ziko katika hatua za mwisho kukusanywa kwenye ngazi za wilaya ili ziwasilishwe mkoani na baadaye ofisi ya Waziri Mkuu.
Mwilapwa alisema tathmini ya awali inaonyesha kuwa athari za mvua hizo ni kubwa kwa mkoa mzima wa Tanga.

Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), Mkoa wa Tanga, Alfred Ndumbaro aliitaja miundombinu iliyoharibika kuwa ni barabara kuu ya Segera -Njiapanda ya Himo eneo la kuanzia Mombo hadi Mkumbara; Mombo –Soni –Lushoto; barabara kuu ya kutoka Tanga hadi Pangani, Maguzoni ambako daraja limeharibika na Kerenge ambako karavati limesombwa na maji.
Pia daraja la Nema Tongoni linalounganisha kati ya Tanga na Pangani limesombwa na maji.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Makamba ambaye pia ni Mbunge wa Bumbuli mkoani Tanga, alisema mabadiliko ya tabia ya nchi na kilimo kisicho endelevu ni miongoni mwa sababu zilizosababisha maporomoko ya udongo yaliyotokea Lushoto.
Makamba alisema jana kuwa mvua imeleta athari na hasa za kimazingira na kwamba, ameshazungumza na wizara husika kwa ajili ya ukarabati wa barabara ikiwamo eneo la Mombo.
“Nimesikitishwa sana kwa sababu Serikali ilitumia fedha nyingi katika ujenzi wa barabara lakini leo hii zimeharibika kutokana na mvua,” alisema Makamba ambaye alieleza kuwa alikuwa akijiandaa kwenda Tanga.
Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: