Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohamed Aboud Mohamed alisema hayo wakati akijibu maswali ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi mjini Zanzibar kuwa pamoja na wajumbe wa baraza hilo kutaka kuanzishwa kwa sheria ya adhabu hiyo, lakini sheria za kukabiliana na suala hilo zipo nyingi na zinafanya kazi vizuri.
Alisema kuwa jambo linalohitajika ni usimamizi mzuri wa sheria hizo ili kuona kila mhusika wa uingizaji, usambazaji pamoja na watumiaji wa dawa hizo wanaadhibiwa kwa mujibu wa sheria.
Hata hivyo alisema kuwa janga la dawa za kulevya ni kubwa hivyo nguvu ya pamoja kati ya viongozi, vyombo vya sheria pamoja na wananchi zinahitajika ili kulitokomeza.
Aboud alisema kuwa mikakati maalum inafanyika ili kuona tatizo hilo linapatiwa dawa mahususi ya kulimaza ikiwamo kuandaa doria maalumu kwa vyombo vya ulinzi katika maeneo ya bandari, viwanja vya ndege na mengine ambayo hutumika kimagendo kwa ajili ya upitishaji.
Mwakilishi wa viti maalumu, Hidaya Ali Makame alisema kuwa jitihada kubwa kwa Jeshi la Polisi zinahitajika ili kuona wanzibari wanaziba mianya yote ya usambazaji na uingizaji wa dawa hizo.
“Nadhani sasa nguvu zielekezwe zaidi katika mapambano kuliko kujenga nyumba kwa ajili ya watumiaji wa dawa za kulevya, kwani hizo nyumba naona kama hazisaidii kitu maana vijana wanaowekwa humo wakitoka tu wanarudia tena utumiaji wa dawa hizo, kumbe tunasahau kudhibiti hao waletaji na waangiziaji, kwani tukifanikiwa kuwatia mikononi hao tutakuwa hatuna mtumiaji hata mmoja,”alisema.
Mtumwa Suleiman Makame ambaye ni mwakilishi wa viti maalumu alisema ili kudhibiti wimbi la vijana wanaotumia dawa za kulevya vijiwe vyote wanavyokaa viondolewe kwa kuwa vinachangia kuwashawishi wengi wao kujiunga katika matumizi ya dawa hizo.
0 Post a Comment:
Post a Comment