Rais Buhari aonekana hadharani kwa mara ya kwanza


  • 5 Mei 2017
Rais wa Nigeria, Mohammadu Buhari
Rais wa Nigeria, Mohammadu Buhari
Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari ameonekana hadharani kwa mara ya kwanza kwa zaidi ya wiki moja, hiyo ni kulingana na taarifa katika mtandao wa kijamii kutoka kwa mmoja wa wasaidizi wake.
Mkanda mfupi wa video, unamuonyesha Bw Buhari akizungumza na watu, baada ya kutoka msikitini kwa swalah ya Ijumaa katika Ikulu ya Rais.
Rais Buhari akiwa msikitini IjumaaHaki miliki ya pich
Image captionRais Buhari akiwa msikitini Ijumaa
Kumekuwepo na tetesi kuhusiana na afya ya Rais huyo, kwani hajaonekana hadharani tangu aliporejea Nigeria kutoka kwa ziara ya matibabu ya wiki saba nchini Uingereza, alipokwenda kutibiwa ugonjwa ambao bado haujajulikana.
Pia hajahudhuria mikutano mitatu ya baraza la mawaziri, na hakuhudhuria maombi ya ijumaa msikitini juma lililopita.
Lakini washauri wake wanasema kwamba, alikuwa akipumzika huku akifanya kazi akiwa nyumbani.
Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: