Sheria ya ndoa 1971 kurekebishwa


   

 8 Mei 2017

WIZARA ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto imesema inatarajia kupendekeza kwenye marekebisho ya Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971, umri wa kuolewa sasa uwe miaka 18 badala ya 14 wa sasa.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu alibainisha hayo  wakati akijibu hoja za wabunge wakati wa kupitisha bajeti ya wizara yake ya Sh 1,115,608,772,090 kwa mwaka wa fedha 2017/2018.
Alisema atakwenda kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali hivi karibuni kwa ajili ya marekebisho hayo ili umri wa kuolewa ubadilishwe uwe miaka 18 badala ya miaka 14 lakini atashawishi kwa sababu maalumu mtoto aruhusiwe kuolewa chini ya miaka hiyo 18.
“Nchini Bangladesh, nchi ya kiislamu hivi Januari mwaka huu imerekebisha sheria yao ya ndoa na kuwa umri wa kuolewa miaka 18 lakini kwa sababu maalumu kama mimba, mtoto anaweza kuolewa chini ya umri huo, nami hivi karibuni nitakutana na Mwanasheria Mkuu na nitawashawishi wenzangu tufuate hivyo kama Bangladeshi,”alisema.
Waziri huyo ameziagiza halmashauri zote nchini kupeleka maoteo ya dawa ifikapo Januari 30 ya kila mwaka ili kuiwezesha Bohari ya Dawa(MSD) kufikisha dawa mapema kwenye halmashauri zao tofauti na sasa halmashauri hizo zinachelewesha maoteo hayo.
“Nataka nipimwe kwa upatikanaji wa dawa, aina 135 za dawa zitapatikana kwa asilimia 95 mwaka huu…madaktari andikeni dawa zilizopo hospitalini kwa wagonjwa na si zilizopo kwenye maduka yenu ya dawa na hili tutalisimamia,”alisema.
Kuhusu huduma kwa watoto alisema wizara yake imetoa mchoro mpya wa hospitali ambapo sasa ni lazima kila hospitali ya mkoa nchini iwe na chumba cha kulaza watoto na hakuna ramani itakayopitishwa isiyokuwa na chumba hicho cha kulaza watoto.


Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: