Mabaki ya ndege ya Myanmar na miili yapatikana baharini


 8 Juni 2017

Ndege ya Y-8 sawa na iliyoanguka baharini
Ndege ya Y-8 sawa na iliyoanguka baharini
Jeshi la Burma linasema kuwa mabaki yamepatikana baada ya ndege ya jeshi kutoweka ikiwa na watu 122.
Mabaki ya ndege na maiti zimepatikana katika bahari ya Andaman, kwa mujibu wa taarafa iliyotolewa na jeshi.
Ndege hiyo aina ya Y8 iliyotengezwa nchini China ilikuwa na wahudumu 14 pamoja na wanajeshi 106 na familia wakiwemo watoto.
Ndege hiyo ilikuwa safarini kutoka Myeik ikielekea Yangon.
Ndege hiyo ilikuwa imefanya safari ya nusu saa wakati ilipoteza mawasiliano siku ya Jumatano.
Ndege hiyo ilinunuliwa kutoka China mwezi Machi mwaka uliopita na tayari ilikuwa imeruka kwa saa 809.
Mynmar imekumbwa na ajali kadha za ndege miaka ya hivi karibuni.
Mwezi Februari mwaka 2016 watu watano waliokuwa wakisafiri wakitumia ndege ya jeshi walifariki wakati ndege hiyo ilianguka kwenye mji mku wa Nay Pyi Taw.
Miezi mitatu baadaye maafisa watatu waliuwawa wakati helikopta ya jeshi ilianguka kati kati mwa Mynmar.
Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: