Mwanasiasa wa Kenya GG Kariuki afariki dunia



30 Juni 2017

GG Kariuki, Kenyatta na Kabogo mwaka 2012
Bw Kariuki (kwanza kushoto) alikuwa wa chama cha Rais Kenyatta. Kulia ni Gavana wa jimbo la Kiambu William Kabogo.

Mwanasiasa wa muda mrefu Kenya, Godfrey Gitahi Kariuki, maarufu kama GG Kariuki amefariki dunia.
Bw Kariuki amekuwa seneta wa jimbo la Laikipia mashariki mwa mji mkuu wa Nairobi.
Seneta Kariuki alikuwa ndiye mbunge pekee aliyekuwa katika bunge la wakati wa uhuru Kenya ambaye alikuwa bado mbunge.
Alichaguliwa mara ya kwanza bungeni Mei 1963 na akahudumu kama mbunge mfululizo kwa miaka 20 kabla ya kupoteza kiti katika uchaguzi wa 1983.
Alihudumu mihula kadha kama mbunge wa eneo bunge la Laikipia Magharibi na alihudumu kama waziri serikali za Mzee Jomo Kenyatta na Daniel arap Moi.
Rais Uhuru Kenyatta ametuma salamu za rambirambi na kumweleza Bw Kariuki kama kiongozi aliyechangia katika ukombozi na ukuaji wa Kenya kama taifa.
Bw Kenya amesema licha ya umri wake aliendelea kuchangia siasa na mustakabali wa taifa na alikuwa na usemi wa busara wakati wa mizozo na majibizano kuhusu masuala ya kitaifa.
"Alichangia katika kutatua mizozo ya maskwota, hasa Laikipia na pia alitetea haki za Wakenya wote alipohisi kwamba zinakandamizwa na waliokuwa mamlakani," Rais Kenyatta amesema.


Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: