Watu 50 waambukizwa kipindupindu hotelini Nairobi




23 Juni 2017

Nairobi, Kenya
Nairobi, Kenya
Takriban watu 50 wameambukizwa ugonjwa wa kipindupindu kwenye hoteli inayoandaa mkutano wa afya kwenyr mji mku wa Kenya Nairobi.
Maafisa wanaonya kuwa huenda idadi ya walioambukizwa ikaongezeka. Wanasema kuwa wale wote walioambukizwa ugonjwa huo wamelazwa hospitali moja mjini Nairobi.
Chanzo cha ugonjwa huo bado hakijulikani lakini mara nyingi husambaa kwa njia ya chakula na maji.
Mwezi uliopita watu watano walikufa kutokana na ugonwa wa kipindupindu na kulazimu utawala kuweka vituo vya ukaguzi kote mjini Nairobi.

Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: