Marekani na Uingereza wamejitolea kusaidia katika uchunguzi wa mauaji ya kutatanisha ya kaimu mkurugenzi wa masuala teknolojia wa tume ya uchaguzi na mipaka nchini Kenya IEBC, kabla ya kufanyijka kwa uchaguzi mkuu.
Gazeti la Daily Nation lilisema kuwa balozi wa Marekani nchi Kenya Robert Godec na wa Uingereza Nic Hailey, walilaani mauaji hayo na kuongeza kuwa wanakaribisha kujitolea kwa serikali katika kuchunguza kisa hicho.
Chris Msando alikuwa msimamizi wa mifumo ya kompiuta kwenye uchaguzi ambao utaandaliwa Jumanne, mifumo ambayo ingezuia wizi wa kura.
Mwili wa Bwana Msando ulipatikana kwenye chumba kimoja cha kuhifadhia maiti jijini Nairobi jana Jumatatu.
Kisa hiki kinatokea ikiwa imesalia juma moja kabla ya kuandaliwa uchaguzi mkuu nchini Kenya ambao utafanyika tarehe 8 Agosti.
Polisi wanasema kuwa mwili Msando pamoja na wa mwanamke ambaye hakutambuliwa, ilipatikana eneo la Kikuyu lililo viungani mwa mji wa Nairobi na kupelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha City Mortuary.
Mawasiliano ya mwisho kutoka mwa Musando aliyafanya siku ya Jumamosi mwendo wa saa tisa alifajiri kupitia ujumbe wa SMS kwa mmoja wa wafanyakazi wenzake.
0 Post a Comment:
Post a Comment