China yaiwekea vikwazo Korea Kaskazini

ZAKACHEKA.BLOGSPOT.COM

23 Sep 2017

China yaiwekea vikwazo Korea Kaskazini
Magari ya kubeba mafuta kotoka China Kueleka Korea Kaskazini
Uchina imeimarisha vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini, ambapo imetangaza usitishaji wa ununuzi wa nguo kutoka Korea kaskazini mbali na uuzaji wa mafuta kwa taifa hilo kuanzia leo na baada ya muda fulani.
Hatua hiyo inaambatana na maagizo ya vikwazo yaliyowekwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa siku 11 zilizopita.
Wachanganuzi wanasema kuwa vikwazo hivyo vitaathiri sana raia wa Korea Kaskazini iwapo vitatekelezwa kwenye mpaka kati ya mataifa hayo ambao hauna doria ya kutosha.Rais Kim Jong Un wa KOrea kaskazini amesema kuwa rais Trump atalipia kauli zake katika mutano wa umoja wa mataifa
Rais Kim Jong Un wa Korea kaskazini amesema kuwa rais Trump atalipia kauli zake katika mutano wa umoja wa mataifa
Utengenezaji wa nguo ni huduma muhimu ya pili inayoletea Korea Kaskazini fedha za kigeni na sehemu nne kwa tano ya nguo hizo hupelekwa Uchina.
Inakisiwa kuwa zaidi ya watu 100,000 wanafanya kazi katika sekta hiyo nchini Korea Kaskazini.
Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: