26 Sep 2017
Polisi nchini Kenya wametumia rungu na gesi ya kutoa machozi kuvunja maandamano katika makao makuu ya tume ya uchaguzi IEBC mjini Nairobi.
Waandamanaji wamekuwa wakitaka kufutwa na kuchukuliwa hatua za kisheria maafisa wa vyeo vya juu wa IEBC, kufuatia kufutwa kwa uchaguzi wa urais mwezi uliopita wakidai kuwa maafisa hao walimpendelea Rais Uhuru Kenyatta.
Kiongozi wa upinzani Raila Odinga anailaumu tume ya IEBC kwa kumpendelea Rais Uhuru Kenyatta na chama kinachotawala cha Jubilee na kusema kuwa hawezi kugombea kwenye marudio ya uchaguzi iwapo maafisa hao hawafunguliwa mashtaka.
Mkurugenzi mtendaji wa IEBC Ezra Chiloba, amekataa wito wa kumtaka ajuzulu na anasema amejitolea kutekeleza majukumu yake.
Siku ya Jumanne mamia kadha ya wafuasi wa Odinga walikusanyika nje ya ofisi za tume ya IEBC wakiwa na mabango yenye maandishi "Chiloba nje."
0 Post a Comment:
Post a Comment