26 Sep 2017
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, ametoa wito wa kutaka kubuniwa kikosi cha pamoja cha jeshi kama sehemu ya maono yake ya siku za usoni kwa muungano huo.
Bwana Macron alipendekeza kuwa kikosi hicho kipya kitakuwa ni sehemu ya Nato.
Aliingia madarakani mwezi akiahidi kuchangia udhabiti Ulaya.
Wakati wa hotuba kuu kwenye chuo cha Sorbonne mjini Paris, Bw Macron alisema anataka muungano wa Ulaya kuboresha mifumo yake ya ulinzi kwa kubuni jeshi la pamoja.
Hakutoa taarifa zaidi lakini alisema kuwa kikosi hicho kitakuwa sehemu ya Nato na kinatajiwa kuanza huduma ifikapo mwaka 2020.
Nchi kadha za Muungano wa ulaya sawa na kamishina wa tume ya Ulaya Jean-Claude Juncker, awali wamesema kuwa kunastahili kuwepo jeshi la pamoja na Ulaya kukabiliana na Urusi na vitisho vingine.
Lakini Uingereza imeonya kuwa hatua hiyo itahujumu kikosi cha Nato
0 Post a Comment:
Post a Comment