NDOA YA JINSIA MOJA: WAZIRI MKUU WA AUSTRALIA AUNGA MKONO

ZAKACHEKA.BLOGSPOT.COM

10 Sep 2017

Protestors gathering in central Sydney, thousands are seen with signs and rainbow flags
Zaidi ya watu 20,000 walikusanyika mjini Sydney kwenye kampeni kabla ya kura ya maoni isiyo rasmi ya kubadilishwa sheria za ndoa nchini Australia.

Viongozi wa siasa nchini Australia akiwemo waziri mkuu Malcolm Turnbull, wameunga mkono kampeni inayopigia debe ndoa ya jinsia moja.

Bwana Turnbull alijitokeza kwa ghafla na kutoa hotuba wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo huko New South Wales.
Kiongozi wa upinzani Bill Shorten kisha akahutubia umati kwenye mkutano mkuu.
Kura hiyo ya kubadilisha sheria ya ndoa inapigwa kwa njia ya posta kuanzia Septemba 12 na matokeo yakitarajiwa mwezi Novemba.Malcolm Turnbull in front of an Australian flag
Awali waziri mkuu alisema kuwa yeye binafsi atapiga kura kuunga mkono ndoa ya jinsia moja

Haki mili

Kura hiyo haitakuwa na uwezo wa kuhalalisha ndoa ya jinsia moja, lakini itachangia kura kupigwa bungeni ikiwa asilimia kubwa na watu nchini Australia wataunga mkono mabadiliko hayo.
Awali waziri mkuu alisema kuwa yeye binafsi atapiga kura kuunga mkono ndoa ya jinsia moja lakini hajafanya kampeni hadharani kabla ya hotuba ya kungashaza leo Jumapili.
Bwana Turnbull alisema kuwa nchi zingine 23 tayari zimehalalisha ndoo ya jinsia moja.
Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: