TEMBO WATANO WAOKOLEWA KATIKA SHIMO SINGIDA

ZAKACHEKA.BLOGSPOT.COM
30 Sep 2017

Ndovu waliokwama wanusuriwa Tanzania
Ndovu wanne wakiwemo watoto wawili waliokolewa lakini ndovu mmoja mkubwa alifariki kutokana na ukosefu wa maji kulingana na chombo cha habari cha China Xinhua.
Kampuni ya ujenzi ya China Sinohydro imewapeleka wahandisi wake na tingatinga katika eneo la kuhifadhi wanyama pori la Rungwe katikati ya Tanzania ili kuwaokoa tembo watano waliokwama katika shimo
Kulingana na duru kutoka kwa kampuni ya Sinohydro, baadhi ya wakaazi wa manyoni eneo la Singida waliwaita wafanyikazi wa kampuni hiyo kuwasaidia tembo hao yapata kilomita 40 kutoka katika hifadhi hiyo.
Saa moja baadaye, waokoaji hao wa China waliwasili katika eneo hilo na kuanza uokoaji baada ya kupata ruhusa kutoka kwa gavana wa eneo hilo na wasimamizi wa hifadhi hiyo.
Kulingana na Xhinua wakaazi wa eneo hilo wamesema kuwa wanyama hao walianguka katika shimo hilo walipokuwa wakitafuta maji.
Shimo hilo lilikuwa dogo na kuwalazimu ndovu hao kuanza kusukumana kwa hofu.
Baada ya saa tano za kazi ngumu ya kuwanusuru, ndovu mmoja mkubwa na watoto wake walikuwa wa kwanza kutolewa katika shimo hilo.
Ndovu wengine wawili walifuatia baadaye lakini mmoja mkubwa akaaga dunia.

TUFUATE FACEBOOK@ZAKACHEKA.HABARI

Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: