SAMSON MWIGAMBA ACT AJIUZULU WADHIFA WAKE

ZAKACHEKA.BLOGSPOT.COM
16 Oktoba 2017


 Mwenyekiti wa Kamati ya Kampeni  na Uchaguzi Taifa na  Mjumbe wa Kamati Kuu wa Chama cha Wazalendo ACT , Samson Mwigamba amejiuzulu  wadhifa wake leo Oktoba 16.
Mwigamba amesema kwamba ameamua  akae pembeni ili awe na nafasi nzuri ya kuwahoji vizuri viongozi wa chama chake hivyo ameamua  kubaki kuwa mwanachama mwema.
"Nimeamua kukaa kando kwani tumekuwa hatukubaliani baadhi ya mambo ndani ya Chama hasa Kiongozi wetu," amesema Mwigamba na kuongeza:
"Wacha nikae pembeni niwe mwanachama ili niwe na nafasi ya kuwahoji  vizuri viongozi wetu masuala mbalimbali na nitabaki kuwa mwanachama mwema’’ amesema
Katika barua yake ya kujizulu Mwigamba ambayo amemuandikia kiongozi wa  chama hicho amesema kwamba ‘’Mnamo Aprili 25,2016 nilipokuwa nang’atuka ukatibu mkuu, nilipotoa nasaha zangu mbele ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya chama nilisema ,”salama ya chama chetu ni kubaki kwenye misingi ya uanzishwaji wake’’
Anasema haikuwa bahati mbaya bali alimaanisha kwasababu  alishaanza kuona mwelekeo wa baadhi ya viongozi wa chama wanachepuka nje ya chama.
Amesema baada ya hapo amekuwa akiwalalamikia sana viongozi  ambao wameacha misingi na mambo ya msingi yaliyowafanya waanzishe chama.
Amesema kwamba ‘’kwa sababu hali hiyo inazidi kuongezeka jambo ambalo mimi binafsi naamini ndiyo sababu hasa  Profesa Kitila Mkumbo akaamua kujivua uanachama.
Hivyo  baada ya kutafakari sana nimeamua kujitenga na uongozi wa sasa wa chama ili niwe huru kuwahoji nyinyi viongozi kwa kauli ,matendo na maamuzi yenu ndani ya chama nikiwa mwanachama wa kawaida.
 Tufuate facebook: zakacheka.blogspot.com na u-download App yetu huko

Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: