Emmerson Mnangagwa kumrithi Robert Mugabe kama rais.

ZAKACHEKA.BLOGSPOT.COM

Ni siri iliyofichuka nchini Zimbabwe kwa miaka mingi kwamba Emmerson Mnangagwa alitaka kumrithi Robert Mugabe kama rais.
Na Bwana Mugabe anaonekana kuwa amekuwa akichezea hisia zake - na amekuwa akimpandisha vyeo katika chama tawala cha Zanu-PF party na hata katika serikali, jambo lililozusha uvumi kwamba Bwana Mnangagwa ''ndie mrithi wake'' lakini baadaye alimshusha cheo huenda baada ya kuonyesha azma yake wazi pengine kupita kiasi.
Lakini baada ya kufutwa kazi, inaonekana kana kwamba subra ya Mnangagwa anayefahamika kwa jina maarufu la "mamba" ilikwisha.
Baada ya kufutwa kazi na Bwana Mugabe kumpuuza na kumshutumu hadharani kwa "usaliti", wafuasi wake katika jeshi waliingilia kati kwa niaba yake.
Lakini yeyote mwenye matumaini kwamba urais wa Mnangagwa utamaliza ukiukaji wa haki za binadamu nchini Zimbabwe huenda anajitanganya .
Bwana Mnangagwa (kushoto) akiwa pamoja na rais MugabeHaki miliki ya pichaAFP
Image captionBwana Mnangagwa (kulia) amekuwa akikabiliwa na mabadiliko katika maisha yake ya kisiasachini yau tawala wa rais Mugabe
Wakosoaji wake wanasema kuwa Kiongozi huyo mkongwe mwenye umri wa miaka 71- ana damu mikononi mwake.
uhusiano wake na Kongo
Bwana Mnangagwa alizaliwa katika jimbo la Zvishavane na anatoka katika kabila dogo ambalo ni sehemu ya jamii ya Washona
Watu wa Kabla la Karanga ni kabila kubwa katika jamii ya Washona na baadhi wanahisi ni wakati wao sasa wa kuingia madarakani, kufuatia miaka 37 ya utawala wa raia Mugabe anayetoka katika kabila la Zezuru.
Tuma habari WhatusApp 0625966236
Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: