Mamlaka nchini Indonesia imetangaza hali ya tahadhari kubwa kufuatia kuwepo dalili za kutokea mlipuko mkubwa wa Volcano katika mlima wa Agung.
Uwanja wa ndege wa kipekee katika kisiwa hicho maarufu cha utalii cha Bali umefungwa.
Majivu na moshi wa Volcano hiyo imefikia urefu wa zaidi ya mita 3000 juu ya mlima huo hali iliyosababisha giza.
Mlima huo uitwao Agung ulirusha majivu mengi na kutandaza mvuke na moshi mwingi mara ya pili katika kipindi cha wiki moja.
Maafisa wamehimiza na kuwasaidia maelfu ya wakaazi na watalii kulihama ene hilo na kwenda kwingine.
Mwaka 1963 mlima huo ulilipuka na kusababisha vifo vya takriban watu 1,600.
0 Post a Comment:
Post a Comment