Mugabe na mkewe Grace hawajaonekana katika sherehe za kuapishwa Emerson Mnangagwa

ZAKACHEKA.BLOGSPOT.COM=>
Robert Mugabe na mkewe Grace walikosa kuhudhuria sherehe ya kuapishwa kwa rais Emmerson Mnangagwa baada ya wananiasa hao kukubaliana kwamba Mugabe anaweza kupumzika.
Sababu kuu ilioteolewa ni kwamba bwana Mugabe alikuwa amechoka.
Mugabe na mkewe Grace hawajaonekana hadharani tangu kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 93 kujiuzulu kama rais kufuatia shinikizo kutoka kwa jeshi na raia.
Hatua hiyo inajiri baada ya Mugabe na mkewe kumfuta kazi rais huyo mpya wakati alipokuwa makamu wa rais kwa madai kwamba alikuwa akipanga njama za kutaka kumuondoa madarakani rais Mugabe
Aliyekuwa makamu wake wa rais Emmerson Mnangagwa amewataka raia wa Zimabwe kusalia watulivu na kuweka amani na kutolipiza kisasi.
Umati mkubwa wa takriban raia 60,00 wa Zimbabwe wakiwemo viongozi wa kimataifa na wanadplomasia walihudhuria sherehe ya kumuapisha Mnangagwa katika uwanja wa michezo wa mjini harare.
Upinzani umemtaka rais mpya kukabiliana na ufisadi.wakati rais Mugabe alipolazimishwa kuondoka madarakani siku ya Jumanne baada ya jeshi kuchukua mamlaka kulikuwa na sherehe matika maeneo tofauti ya taifa hilo.
Tuma habari picha, video za matukio mbalimbali WhatsApp kwa 0625966236
Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: