Marekani:Mahakama kutekeleza zuilio la wageni

ZAKACHEKA.BLOGSPOT.COM
Mahakama kuu nchini Marekani imeamua kuwa toleo la marufuku ya kusafiri ya Rais trump inaweza kutekelezwa kwa ukamilifu.
Huku ikiendelea kukutana na changamoto za kisheria kutoka mahakama za chini.
Nchi sita zinazokutana na zuio hilo ni Iran, Libya, Syria, Yemen, Somalia na Chad.Mahakama za chini tayari zimeruhusu kuzuiwa kwa baadhi ya watu kutoka Korea kaskazini na Venezuela.
Majadiliano Zaidi yatendelea kusikilizwa wiki hii katika mahakama huko San Francisco, California, na Richmond, Virginia.
Huu ni ushindi mkubwa kwa Donald Trump.
Msemaji wa Ikulu ya White Hogan Gidley alisema kuwa White House haikushangazwa na uamuzi wa mahaka ya juu.
Mwanasheria mkuu Jeff Sessions aliutaja uamuzi huo kama ushindi mkubwa kwa usalama wa watu wa Marekani.

Tuma habari picha na video za matukio mbalimbali WhatsApp kwa 0625966236

Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: