Msigwa amefunguka hayo wakati akituma salamu kwa wale ambao wamekuwa wakimrubuni kuhamia CCM na kusema kwamba heshima na dhamana aliyopatiwa na wananchi wa Manispaa ya Iringa ni kubwa mno hivyo kufanya hivyo ni kuuza hadi utu wa wapiga kura.
Msigwa ameweka wazi kwamba amekuwa akipokea simu za vitisho kutoka upande wa chama tawala wakimtaka akubali kupokea ofa yao ya kuhama chama na bila hivyo basi hataweza tena kurudi bungeni baada ya kufika 2020.
"Nikihamia CCM wananchi wa Iringa wachome nyumba yangu na magari yangu. Sikuingia bungeni kwa sababu nataka ghela ila nimeingia kwa sabu kuna hoja kuna agenda na kozi kama chama tunapigania. Mkome kabisa kunipigia simu mimi sina bei itakayonihamisha CHADEMA," amefunguka Msigwa.
Akizungumzia kuhusu alivyokuwa akirubuniwa, Msigwa amesema "Walianza kunipigia kwa kujifanya marafiki zangu na baadae wakaanza kunipanga na kunirubuni kwamba Mzee ananikubali na wala hana shida na mimi hivyo nikiingia CCM nitapata nafasi, nimewakemea na nimeonya wasinipie simu na sasa hivi wameacha ila naahidi wakinipia tena nitawarekodi niwaanike hadharani" I am not that 'cheap' wakatafute wengine," Msigwa ameweka wazi.
Aidha Msigwa amefafanua kwamba hakuuingia bungeni kwasababu anahitaji pesa kwani hata kama asingekuwa Mbunge angeweza kuwa Mkurugenzi wa makampuni na kuongeza kwamba alikuwa na maisha hata kabla ya kuwa mwanasiasa na mbunge.
"Sikuingia Bungeni kwa ajili ya pesa, sipo tayari kurubuniwa kwa maneno matamu wala fedha au ushawishi kuuza utu ambao wananchi wa manispaa ya Iringa wamenipa. Ukiniangalia kwani nashindwa kuwa CEO, naweza kuwa Mkurugenzi wa kampuni yoyote. Mimi nilikuwa na maisha kabla ya kuingia hta bungeni. Sisi bado tupo imara....wacha hivi vivulana viondoke sisi ambao tunajua nini tunakutaka bado tupo imara ndani ya chama" Msigwa.
=> Tuma habari picha na video za matukio mbalimbali WhatsApp kwa 0625966236
0 Post a Comment:
Post a Comment