Marekani: Tunasikitishwa na vitendo vya utekaji na ukatili Tanzania

ZAKACHEKA.BLOGSPOT.COM=>
Ubalozi wa Marekani Tanzania unataka uchunguzi huru kuhusu matukio ya matumuizi ya nguvu dhidi ya harakati za kisiasa za upinzani.
Hii ni baada ya kifo cha mjumbe wa chama cha upinzani CHADEMA, Daniel John tarehe 11 Februari, ambaye mwili wake ulipatikana katika fukwe za bahari ya hindi, jijini Dar es salaam, siku moja baada ya kutekwa ukiwa na majeraha ikiwemo shingo yake kunyongwa na watu ambao hadi saa hawajajulikana.
Marehemu anaripotiwa kutekwa pamoja na mwenzake, Reginald Mallya aliyenusurika na kupatikana akiwa hai akiwa na majeraha kadhaa sehemu za mkononi na kichwani.
Mwenyekiti wa chama cha upinzani CHADEMA, akionesha picha ya marehemu Daniel JohnHaki miliki ya pichaCHADEMA MEDIA/ FACEBOOK
Image captionMwenyekiti wa chama cha upinzani CHADEMA, akionesha picha ya marehemu Daniel John
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwenye mtandao wa balozi wa Marekani, balozi wamesema "Tunatuma salamu zetu za rambirambi kwa familia na marafiki wa marehemu kwa msiba huu."
"Kuongezeka kwa makabiliano ya kihasama na vitendo vya kikatili ni jambo linalotutia wasiwasi na kutusikitisha sana."
Pamoja na hayo ubalozi umetaka "uchunguzi wenye uwazi ili kuwawajibisha wale wote wanaohusika na vitendo hivi vya kikatili kwa mujibu wa sheria za Tanzania."
Tukio hilo limefayika ikiwa ni juma la mwisho la kampeni za uchaguzi mdogo katika majimbo mawili nchini Tanzania ambayo yalipoteza wabunge wake kwa sababu mbalimbali ikiwemo ile ya wabunge wa upinzani kujiuzulu kwa kile walichokiita kuunga mklp0oooono jitihada za Rais Magufuli na serikali ya awamu ya tano.
Kwa upande wake, kamanda wa polisi wa mkoa wa kipolisi wa Kinondoni, Jumanne Murilo, amesema polisi waachwe wafanye uchunguzi kufuatia vitendo hivyo vya utekaji nyara.
Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu akiendelea na mazoezi ya viungo huko nchini Ubelgiji.Haki miliki ya pichaCHADEMA MEDIA/ FACEBOOK
Image captionMbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu akiendelea na mazoezi ya viungo huko nchini Ubelgiji.
Kumekuwa na kinachoonekana kama muendelezo wa vitendo vya mashambulizi dhidi ya wanachama wa upinzani,hivi karibuni nchini Tanzania. Kikubwa kikiwa ni shambulio dhidi mnadhimu mkuu wa chama cha upinzani nchini Tanzania Chadema, Bw Tundu Lissu anayezidi kupata matibabu nchini Ubelgiji baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana jijini Dodoma mwaka uliopita.
Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: