Matokeo Ya Awali: Mtulia aongoza Jimbo la Kinondoni

ZAKACHEKA.BLOGSPOT.COM=>
Matokeo ya awali ya uchaguzi wa ubunge Jimbo la Kinondoni yaliyobandikwa nje ya vituo vya kupigia kura yanaonyesha mgombea wa CCM, Maulid Mtulia anazidi kuongoza katika baadhi ya vituo.

Katika matokeo hayo, Mtulia anafuatiwa na mgombea wa Chadema, Salum Mwalimu huku wa CUF, Salum Rajab Juma akishika nafasi ya tatu lakini kwa tofauti kubwa ya kura.

Baadhi ya matokeo hayo ni kama ifuatavyo; Kituo cha Mbuyuni 3 Kata ya Tandale,  Mtulia amepata kura  53, Juma 3 na Mwalimu 18.

Kituo cha Mashuka 2 Kata ya Tandale, Mwalimu amepata kura 16, Juma 7 na Mtulia 53.

Kituo cha Mashuka 1 Kata ya Tandale, Mtulia amepata kura 59, Mwalimu 14 na Juma 3.

Kituo cha Ofisi ya Mpakani -7 Kata ya Ndugumbi, Mtulia amepata kura 33, Mwalimu 20, Juma 6 na mgombea wa Tadea 1.

Kituo cha Mpakani -3 Kata ya Ndugumbi, Mtulia amepata kura 49, Mwalimu 14, Juma 16 na mgombea wa Tadea 1.

Kituo cha Serikali ya Mtaa Bwawani 4 Kata ya Kijitomyama, Mtulia amepata kura 237, Mwalimu 21 na Juma 1.

Kituo cha Bwawani 01 Kata ya Kijitonyama, Mwalimu amepata kura 23 na Mtulia 100.

Kituo cha Bwawani 2 Kata ya Kijitonyama, Mtulia amepata kura 37, Mwalimu 24 na Juma 1.

Kituo cha Weo 1 Kata ya Makumbusho, Mtulia amepata kura 35, Mwalimu 20 na Juma 3.

Kata ya Sokoni Makumbusho A-1 Kata ya Kijitonyama, Mtulia amepata kura 30, Mwalimu 12 na Ashiri Saidi 1.

Kituo cha Shule ya Msingi Mwananyamala Kisiwani B Kata ya Makumbusho, Mwalimu amepata kura 13, Mtulia kura 39 na mgombea wa UMD 1.

Kituo cha Shule ya Msingi Mwananyamala Kisiwani C 1 Kata ya Makumbusho, Mtulia amepata kura 41, Mwalimu 15 na Juma 9.

Kituo cha Shule ya Msingi Mwananyamala C 2 Kata ya Makumbusho, Mtulia amepata kura 42, Mwalimu kura 21 na Juma 15.

Kituo cha Kijitonyama 2  Kata ya Kijitonyama, Mwalimu amepata kura 20, Mtulia 29 na Juma 1.

Kituo cha Shule ya Msingi Kijitonyama B2 Kata ya Kijitonyama, Mtulia amepata kura 78, Mwalimu kura 24 na Ally Abdallah wa Tadea 1.

Kituo cha Shule ya Msingi Kijitonyama A-2 Kata ya Kijitonyama, Mwalimu amepata kura 24, Mtulia 68 na Ally Abdallah wa Tadea 1.

Kituo cha Shule ya Msingi Kisiwani D 2 Kata ya Makumbusho, Mtulia amepata kura 37, Mwalimu 21 na mgombea wa NRA 1.

Kituo cha Shule ya Msingi Minazini C 1 Kata ya Makumbusho, Mtulia amepata kura 46, Mwalimu 20 na Juma 12.

Kituo cha Ofisi ya Serikali ya Mtaa Kijitonyama 2 Kata ya Kijitonyama, Mtulia amepata kura 25, Mwalimu kura 36.

Kituo cha Ofisi ya Weo-3 Kata ya Kijitonyama, Mtulia amepata 22, Mwalimu 20.

Kituo cha Mwenge Zahanati Kata ya Kijitonyama, Mtulia amepata 19 na Mwalimu 12.

Kata ya Mwenge Zahanati 2 Kata ya Kijitonyama, Mtulia amepata kura 56 na Mwalimu 13.

==Matokeo zaidi yanaendelea kutangazwa
Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: