Mahitaji
- Unga wa ngano 250g (robo kilo)
- Butter 250g (robo kilo)
- Mayai 9
- Baking powder kijiko cha chai1
- kuku wa kusaga vikombe 2
- Chumvi kijiko cha chai 1
- Sukari ⅓ ya kikombe
- Kungu manga ½ kijiko cha chai(sio lazima)
- Mdalasini kijiko cha chai 1
- Curry powder kijiko cha chai 1
- Kitunguu swaumu kijiko cha chai 1
- Tangawizi kijiko cha chai 1
- Chicken stock kijiko ½ cha chai
- Pilipili mtama ½ kijiko cha chai
- Ndimu/limau moja
- Pilipili hoho ½ kila rangi
Jinsi ya kupika
Muoshe kuku wako vizuri asiwe na ngozi, muwekee viungo vyote mbandike jikoni isipokuwa usiweke pilipili hoho.
Mwache achemke na hayo Maji yakikauka muweke pembeni apoe.
Kama utakuwa haujapata kuku wa kusaga umechemsha kuku mzima basi akipoa mnyambue nyambue au msage katika blender,muweke pembeni.
Saga siagi na sukari pamoja na mayai 3,yakichanganyika weka unga na baking powder.
Ikichanganyika vizuri weka katika chombo cha kuchomea,chukua kuku wako changanya na mayai 3 mimina juu ya ule unga wako wa keki uliopo katika chombo cha kuchomea,halafu piga Yale mayai matatu yaliyobakia ya changanye na pilipili hoho miminia juu.
Weka katika oven moto 350.
Baada ya hapo keki yako itakuwa tayari.
Kwa Injili Bofya
0 Post a Comment:
Post a Comment