RC Mnyeti aagiza vigogo watano uchimbaji madini kukamatwa

ZAKACHEKA.BLOGSPOT.COM=>
Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti ameagiza vigogo watano wachimbaji na wanunuzi wa madini ya Tanzanite katika mji mdogo wa Mirerani wilayani Simanjiro na jijini Arusha, kukamatwa na  polisi wakidaiwa kufadhili uchimbaji haramu wa madini hayo.
Jana Februari 8, 2018 kamanda wa polisi Mkoa wa Manyara, Augostino Senga amesema vigogo hao wamekamatwa juzi jioni na kulazwa Kituo cha Polisi Mirerani.
Amesema wanawashikilia baada ya kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa kupata taarifa kuwa, vigogo hao wanashiriki kuwadhamini vijana wanaoingia kwa wizi kwenye migodi ya kampuni ya TanzaniteOne yenye ubia wa asilimia 50 kwa 50 na Shirika la Madini la Taifa (Stamico).
Amesema wanachunguza suala hilo na iwapo vigogo hao ambao majina yao tunayo utakamilika, watafikishwa mahakamani.
Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: