Paul Makonda: Kuna mmoja amesema ametekwa, mi nafikiri wakimalizana nae Iringa watuletee

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amelitaka jeshi la polisi kuendelea kufanya kazi bila kutetereshwa na mtu yeyote na amemuagiza Kamanda Mambosasa na timu yake kuwashughulikia watu wanaotumia lugha za kashfa dhidi ya viongozi wa nchi ambao ni nembo ya taifa.

Pia amewaomba waandishi wa habari kuangalia taarifa wanazozisambaza kwa umma kuhakikisha kuwa ni taarifa ambazo zimethibitishwa na mamlaka husika kwani taarifa nyingi zinazosambazwa zimekuwa zikileta taharuki katika umma.

Hayo ameyasema kufuatia habari zilizosambaa hivi karibuni kuhusu Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi nchini Tanzania ambaye ni Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Abdul Nondo ambaye alipotea siku chache zilizopita na kupatikana akiwa Mafinga.

Amesema kuwa kitendo cha waandishi wa habari kuandika habari ambazo hazijathibitishwa na mamlaka husika huchafua mkoa wa Dar Es Salaam na hivyo ameagiza kijana huyo ashughulikiwe.

”Juzi nimesikia kuna mmoja amesema ametekwa, mi nafikiri wakimalizana nae kule Iringa watuletee huku Dar es salaam, asituchafulie mkoa wetu” amesema Makonda.

Aidha ameomba Mamlaka ya Mawasiliano TCRA, kushughulikia makosa ya kimtandao ili kuhakikisha nchi yetu inabaki katika amani na utulivu.

Download App YETU hapa⬇⬇



Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: