Mamlaka nchini Mexico zimewafungulia mashtaka polisi wanne kufuatia kutoweka kwa wanaume watatu raia wa Italia.
Wanaume hao ambao kwa sasa hawajulikaniwaliko, walionekana mara ya mwisho tarehe 31 Januari eneo la Tecalitlán, katika jimbo la magharibi la Jalisco.
Gavana wa jimbo hilo alisema polisi hao walikiri kuwasalimisha wanaume hao kwa genge moja la wahalifu.
Inadaiwa kwa polisi walidai kuwakamata kwenye kituo cha petroli kabla ya kuwasalimisha.
Ni kipi kinadaiwa kutokea?
Raffaele Russo, 60, mtoto wake wa kiume wa miaka 25 Antonio, na mpwa wake, Vincenzo Cimmino, 29, walikuwa wamesimamisha gari kwenye kitu cha petroli huko Tecalitlán.
Jamaa zao nchini Italia waliwasiliana nao kupitia ujumbe wa Whatsapp wakisema kuwa walikuwa wameshikwa na polisi
Mtoto wa moja wanaume hao aliiambia radio ya Italia kuwa wanaume hao walikuwa wameuzwa kwa genge hilo kwa dola 53 lakini maafisa wanasema hawawezi kuthibitisha hiyo.
Eneo hilo linadhibitiwa na Jalisco New Generation cartel, moja ya magenge ya wahalifu yenye nguvu zaid nchini Mexico.
0 Post a Comment:
Post a Comment