Trump na Kim Jong Un kukutana mwezi Mei

Rais Donald Trump wa Marekani amekubali ombi la Kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong Un la kutaka wakutane mapema ndani ya mwezi mei mwaka huu,na hivyo kuweka historia kufuatia kuwa kutokuwepo rais wa Marekani ambaye amewahi kuonana na kiongozi mkuu wa Korea kaskazini.
Hata hivyo mahala watakapokutana viongozi panasalia kuwa siri kwa sasa,na pia Marekani imesisitiza kuwa pamoja na kukubali ombi hilo la rais Kim Jong Un laini bado vikwazo vitasalia pale pale.
Tangazo hilo la kwamba rais Trump amekubali kukutana na Kim Jong Un,limetolewa na viongozi wa juu wa Korea Kusini uliofika mjini Washington kuwasilisha barua ya ombi hilo kutoka kwa Korea Kaskazini.
Hatua hii iliyofikiwa ya rais Kim Jong Un kulegeza msimamo ni matokeo ya mazungumzo mazito yaliyofanywa wiki chache zilizopita ujumbe wa Korea Kusini kukutana na kiongozi huyo.

Download App YETU hapa⬇⬇


Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: