Watu 225 wanaambukizwa UKIMWI kila siku

Takwimu zinaonesha kuwa Watanzania 225 huambukizwa VVU kwa siku.

Hali hiyo inamaanisha kwamba kwa mwezi watu 6,750 huambukizwa VVU na kwa mwaka ni 81,000.

Takwimu hizo zimetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS), Dk. Leonard Maboko, jana  Jumanne Machi 6, wakati akifungua mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu uandaaji wa programu bora za Virusi vya Ukimwi (VVU) na Ukimwi.

Alisema hali hiyo ni mbaya zaidi kwa vijana wenye umri kati ya miaka 15 hadi 24.

“Asilimia 40 ya maambukizo mapya hutokea kwa vijana wenye umri Kati ya miaka 15 hadi 24 na kati yao wengi ni wanawake.

“Hii inamaanisha kwamba katika hiyo asilimia 40 ya vijana waliopata maambukizi mapya, asilimia 80 ni wanawake,” alisema Dk. Maboko.

Kwa Idadi hiyo tunaona wastani wa maambukizi kwa saa mmoja ni watu 9 au 10 .

Download App YETU hapa⬇⬇

Share on Google Plus

ABOUT BLOGGER INJILI HALISI MINISTRY

Hi! I am Zachary John Bequeker, from Mwanza Tanzania, East Africa.I'm a blogger of ZAKACHEKA NEWS LINE And ZAKKACHEKA INJILI.Contact me +255 625966236 / +255 758590489 or mail on zacharybequeker@gmail.com . Thanks!!!

0 Post a Comment: